Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, katika mkutano huu, wazungumzaji walisisitiza kuwa ushiriki hai wa misikiti barani Ulaya ni miongoni mwa malengo ya mipango ya kielimu, na mojawapo ya mikakati ya mazungumzo ya dini pamoja na shughuli za kiutu.
Kwa hakika, jambo hili ni miongoni mwa nyenzo zenye ufanisi mkubwa katika kupunguza mvutano wa kitamaduni na kuimarisha uelewa wa wazi wa Uislamu wa kweli na Waislamu, na linaweza kuwa chombo chanya na chenye kujenga katika jamii za Magharibi.
Vilevile, viongozi wa Albania waliokuwepo katika mkutano huu walitoa taarifa kuhusu maendeleo ya nchi yao katika uwanja wa ukuaji na ustawi wa misikiti ya Albania, na wakabainisha mipango yao kwa ajili ya nchi nyingine za Ulaya.
Chanzo: Aljazeera
Maoni yako